Ni jana ya tarehe 02/03/2010 katika Jamii yatu tumepata tena rasmi ongezeko la vyama viwili japo ndo kwanza usajili wa Mda rakini kisheria chama akiwezi kufanya shughuli zozote za kisiasa ndani ya Tanzania kama akina usajili wa mda na baadae usajili wa kudumu ndo ufata. Mi nomba niongelee ili la usajili wa mda kwa chama cha siasa, kwanza unakipa nguvu ya kisheria ya kufanya shughuri za kisiasa ndani ya Tanzania na kupatiwa ulinzi pale wanapo itaji lakini la muhimu ni kuruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa kwa maana ya kuanza harakati za kutafuta usajili wa kudumu pia kama chama kinachotambuliwa.
kuanzishwa kwa CCJ kumeleta manenomaneno mengi sana katika jamii yetu moja ikiwa ni kwanza uvumi wa kwamba kuna watu wanataka kujitoa CCM na hivyo wameamua kuanzisha CCJ, pili kuwa ni mkakati wa kuipunguza nguvu CCM na tatu kuna madai kua ni Vajana wameamua kuleta changamoato mpya katika siasa za nchi hii? yote haya ni maswali hambayo moja baada ya jingine yaneweza anza kupata majibu baada ya usajili wa mda wa CCJ.
mi la kwangu ni uongezeko wa vyama na siasa zetu za kiafrika ambazo zimekua zikiongozwa, kusimamiwa na kujengewa misingi ya "ZIMA MOTO TU", kwanza tujiulize ni kwa nini ikiwa imebaki tu miezi takribani tisa tu tufanye uchaguzi ndo kukaja CCJ, wote tunatambua ya kuwa kujenga misingi bola ya chama si kitu cha kulala na kesho ukaamka na kuchukua mchi mimi sithani kama ni sahii hivyo ata kuoa au kuolewa mtu akulupuki leo kapata mchumba leo hii kamtambulisha na kesho akaoa, tunaona Harusi toka kujuani na mwenzi wako mpaka kumchumbia na kumuoa sio chini ya mwaka na zaidi sasa inapo kuja kwenya Nchi tena Nchi kubwa kama Tanzania ebu tutafakali, mi napenda mapindizi ma mabadiliko lakini mapindizi ya kukulupuka watanzania hayatufaahi ni lazima watu tujipange na nchi yetu inaitaji ilo zaidi, CCJ wangekuja mapema wakajipanga taratibu Tanzania ni Nchi na iliyo komaa kisiasa na ivyo kukulupuka sio jambo jema sana.
mimi ningewashauli CCJ mwaka huu wawe watazamaji na wajipange vema wauchukulie kama mwaka wa kujifunza Nchii hii hipo tumezaliwa tumeikuta na tutaiacha.
No comments:
Post a Comment